Sudan imeondolewa vikwazo na Marekani vilivyowekwa na nchi hiyo dhidi ya taifa hilo la Afrika.

Marekani imesema kuwa taifa hilo la Afrika lilikuwa limeanza kuangazia maswala kuhusu kukabiliana na ugaidi pamoja na ukiukaji wa haki za kibinaadamu dhidi ya raia wanaoishi katika jimbo la Darfur.

Uamuzi wa kuiondolea vikwazo na kusitisha vikwazovya kiuchumi wa taifa hilo unajiri baada ya utawala wa Trump mwezi uliopita kuliondoa taifa hilo katika mataifa ambayo raia wake wamewekwa vikwazo vya kusafiri.

Sudan ndio taifa la pekee ambalo liliondolewa katika orodha ya mataifa ambayo raia wake hawatakiwi kuingia nchini Marekani.

Lakini uamuzi huo unaviwacha vikwazo vingine kuendelea kwa sasa ikiwemo vile dhidi ya watu binafsi walio na agizo la kukamtwa kufuatia unyanyasaji uliofanyika katika eneo la Darfur.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *