Rais wa Marekani, Donald Trump amemsifu rais wa China, Xi jinping kwa kuiunga mkono Marekani na jitihada zake za kupambana na mpango wa Nuklia wa Korea kaskazini.

Trump amesema kupata ushirikiano huo wa kupambana na Pyongyang ilikuwa muhimu kuliko kuishinikiza Beijing kuhusu masuala ya biashara.

Rais Donald Trump amesema aliamini kuwa Rais Xi alikuwa akiishinikiza Korea kaskazini, ikitaka, mazungumzo yafanyike kuhusu silaha za Nuklia za Kim Jong Un

Trump ametahadharisha kuwa mgogoro wowote wa kijeshi na Korea kaskazini unaweza kugharimu maisha ya mamilioni ya watu.

Aliyasema hayo kwenye mahojiano na chombo cha habari cha CBS cha Marekani ambapo alizungumzia hali ya mvutano iliopo kati ya nchi yake na Korea kaskazini.

Trump amesema rais wa Korea kkaskazini , Kim Jong Un ameendelea kubaki kwenye utawala wa Korea kaskazini, ingawa wamekuwepo wale ambao wangeweza kumpinga

Siku ya jumapili,Kiongozi huyo wa Marekani alizungumza na Mawaziri wakuu wa Thailand na Singapore kujadili namna ya kuishinikiza Serikali ya rais wa Korea kaskazini, Kim Jong.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *