Rais wa Marekani, Donald Trump amependekeza kunguza fedha za misaada kwa Umoja wa Mataifa na shirika la misaada la USAid.
Trump amepanga kuongeza matumizi ya jeshi hadi kufikia dola bilioni 54 kwa kupunguza kiwango katika maeneo mengine.
Amependekeza kuondolewa kwa msaada wa dola milioni $28.2 kwa Africa Development Foundation, shirika la Marekani ambalo hutoa ruzuku hadi ya $250,000 kwa jamii na biashara ndogo ndogo katika nchi zilizopo chini ya jangwa la Sahara.
Rasimu hiyo ya bajeti kama ikipita itaanza kufanya kazi mwezi October inaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa mpango wa chakula duniani (WFP).
Kupungua kwa bajeti hiyo kunaamisha kuwa mashirika ya kulinda amani na yale ya shughuli za kibinadamu yatapaswa kupanga upya bajeti zake.
Marekani huchangia takriban dola bilioni 10.4 kwa mashirika ya kimataifa ambapo dola bilioni $8.8 huenda kwa Umoja wa Mataifa.