Marekani itafungua ubalozi wake mpya mjini Jerusalem hatua ambayo imesifiwa na Israel na kulaaniwa na Wapalestina ambao wanakusanyika kwa maandamano makubwa.
Maafisa wa vyeo vya juu kutoka Marekani watahudhuria sherehe hiyo leo akiwemo binti ya Rais wa Marekani Donald Trump Ivanka na mumewe Jared Kushner.
Uamuzi wa Trump wa kuhamisha ubalozi huo kutoka Tel Aviv umegadhabisha Wapalestina amboa wanadai eneo la Jerusalem Mashariki ni mji wao mku wa badaye.
Israel ilichukua udhibiti wa eneo la Jurusalem mashariki mwaka 1967 wakati wa vita vya Mashariki ya kati, na inahutaja mji huo kuwa wake na usiogawanwa
Hatua hiyo ya Trump ya mwaka uliopita ya kuutambua mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel ilivunja msimamo wa wastani wa Marekani kwa suala la mji huo na kwenda kinyume na misimamo ya nchi zingine duniani.
Ubalozi wa mdogo utaanza kutoa huduma kuanzia leo Jumatatu kwenye jengo la ofisi za ubalozi mjini Jerusalem.
Eneo lingine kubwa litatafutwa baadaye wakati ubalozi wote utahama kutoka mji wa Tel Aviv.
Sherehe za ufunguzi zilifanywa mapema ili ziweze kuenda sambamba na sherehe za miaka 70 za kuanzishwa taifa la Israel.
Rais Trump anatarajiwa kuhutubia wale ambao watahudhuria sherehe hiyo kwa njia ya video.