Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Jay Melody amefunguka na kukiri kuwa mapenzi ni kitu kinachochukua nafasi kubwa kwenye maisha yake ya kila siku.

Kupitia akaunti yake ya Instagram ameandika “Kimsingi mapenzi yanamaanisha kuwa na upendo usioyumba, usioweza kuvunjika na usio na kifani na kujitolea kwa Mpenzi wako.

Pia ameandika Kuna wakati Upendo/Mapenzi yanaweza yakawa sababu ya Wewe kubadilisha Tabia, Muonekano na hata mambo mengi ambayo hukuwahi kuwaza kama yangeweza kubadilika kwa kasi namna hiyo.

Unapofanikiwa kupata mtu anayeweza kuziendesha vyema fikra, mawazo, moyo pamoja na Maisha yako kwa ujumla katika njia chanya basi Huna la ziada zaidi ya kumjaza Upendo, Kumpa heshima na kumfanya kuwa wako siku zote za Maisha yako.

Ameongeza kwa kuandika Mapenzi yana kila Aina ya changamoto ila Kubwa zaidi Endapo unapoweza kufanikiwa kupata mtu ambaye licha ya changamoto zote mnazopitia akaamua kutulia na wewe kuwa upande wako basi ni jambo ambalo unatakiwa kulizingatia sana, Mpatie kila linalowezekana aendelee kuwa kando yako.

Binafsi mapenzi yamechukua nafasi kubwa sana kwangu, sikuwahi kufikiria kama nitaweza kubadilika namna hii na yote hayo ni MAPENZI MAPENZI.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *