Jumuiya ya Ulaya na Marekani zimeweka vikwazo dhidi ya maofisa wakubwa wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa kuhusika na mauaji ya waandamanaji waliotaka Rais Joseph Kabila kuachia madaraka.

Jumuiya ya Ulaya imewataja maofisa saba wa usalama wakiwemo makamanda wa jeshi pamoja na wa polisi na kiongozi wa ulinzi wa Rais Kabila.

Marekani kwa upande wake wamewataja waziri wa mambo ya ndani wa DRC na mkuu wa intelijensia.

Serikali ya Congo imetaja vikwazo hivyo kuwa sio halali.

Mamia ya watu waliuawa wakati wa maandamano yalioanza mwezi Septemba baada ya Rais Kabila kutangaza kusitishwa kwa uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *