Waziri mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wamiliki wa kiwanda cha kutengeneza mbolea cha Minjingu mkoani Manyara kumuandikia barua Rais Magufuli baada ya kubaini wanatumia mifuko yenye nembo ya Kenya.

Majaliwa amesema kuwa anataka nakala ya barua hiyo kabla ya Jumatano atakapomaliza ziara yake mkoani humo.

Mbolea zinazozalishwa kwenye kiwanda hiko kilichopo mkoani Manyara.
Mbolea zinazozalishwa kwenye kiwanda hiko kilichopo mkoani Manyara.

Waziri mkuu ametoa agizo hilo jana baada ya kutembelea kiwanda hicho kilichopo Wilayani Babati mkoani Manyara ambapo amebaini hali hiyo kwenye kiwanda hicho cha kuzalisha mbolea.

Pia waziri mkuu amesema kuwa atamuagiza waziri wa viwanda na biashara, Charles Mwijage apeleke wanasheria wake na wataalamu kutoka tume ya Ushindani wa kibiashara ili kuangalia hatua gani zinapaswa kuchukuliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *