Bondia kutoka Ufilipino, Manny Pacquiao anatarajia kupambana na Bondia muingereza, Amir Khan ifikapo Aprili 23 mwaka huu.
Pigano hilo litaandaliwa baada ya mashabiki wa Pacquaiao kwenye mtandao wa Twitter
Khana wa umri wa miaka 30 amethibitisha pigano hilo licha ya Pacquaiao kusema kuwa huenda pigano lake likaandaliwa Milki ya nchi za kiarabu, eneo litakaloandaliwa bado halijatangazwa.
Akiongea kwa njia ya video Khan anasema Uingereza, Dubai au Marekani ni kati sehemu ambapo pambano hilo litafanyika.
Pigano la mwisho la Khan lilifanyika mwezi Mei mwaka 2016 wakati alipomshinda kwa Knock out raia wa Mexico Saul “Canelo” Alvarez.