Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametaja orodha ya majina 65 ya awamu ya pili ya wanaohusika na uuzaji wa madawa ya kulevya.
Makonda amewataja Mbunge wa Hai Freeman Mbowe, Mfanyabiashara mkubwa nchini, Yusuf Manji na Mchungaji Josephat Gwajima wametajwa kwenye orodha ya pili.
Wengine waliotajwa na Makonda amemtaja pia mbunge wa zamani wa Kinondoni, Iddi Azan na mfanyabiashara maarufu wa nguo, Hussein Pamba Kali kwenye orodha hiyo.
Makonda amesema orodha hiyo kuwa ni ya wale ambao wanahisishwa na biashara hiyo haramu na wengine wana taarifa muhimu zinazoweza kuwasaidia polisi kuwatia nguvuni vinara wa biashara hiyo.
Wengine walotajwa kwenye orodha hiyo ni wamiliki wa Slipway na Yatchy Club ambao wote wanatakiwa kulipoti kituo cha polisi siku ya Ijumaa.