Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo imehairisha kesi inayomkabili aliyekuwa mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji na wenzake watatu.
Kesi hiyo imehairishwa kutokana na Manji kutofika Mahakamani hapo kutokana na kuhudhuria kesi nyingine mahakama kuu.
Kesi hiyo inayoendeshwa na Hakimu, Huruma Shaidi ilikuwa isikilizwe leo lakini Manji hakufika mahakamani hapo kwa kile kilichoelezwa na mawakili wake kuwa ana kesi nyingine leo katika Mahakama Kuu ya Tanzania.
Manji anakabiliwa na mashtaka saba na watuhumiwa wenzake, yakiwemo ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya JWTZ, ukiwemo wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) na wa Commanding Officer Korogwe,.
Kesi hiyo imehairisha mpaka Agosti 9 mwaka huu itakapotajwa tena kwa ajili ya kusikilizwa mahakamani hapo.