Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP, Simon Sirro amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumteuwa kuwa mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.

Kamanda Sirro amesema hayo baada ya kumaliza kuapishwa kushika wadhifa huo Ikulu jijini Dar es Salaam na kuwa mkuu mpya wa jeshi la Polisi nchini akichukua nafasi ya Ernest Mangu.

Sirro amesema kuwa Rais Magufuli ameona utendaji kazi wake akiwa kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam kwa kupigana na wahalifu katika jiji la Dar es Salaam ambapo sasa uhalifu umepungua.

Amesema kuwa Rais Magufuli amemwamini na kumkabidhi wadhifa huo ili awatumikie Watanzania huku akihaidi kutomuangusha katika utendaji wa kazi yake.

Sirro amesema kuwa “Tuombeane tu ndugu yangu hii nafasi si ndogo ni kubwa kwa Jeshi la Polisi, hivyo naomba ushirikiano kutoka kwenu na mengi nitaongea kesho.

Kwa upande wake Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Richard Mbunda alisema uwajibikaji wa Sirro ndiyo chanzo cha kuteuliwa na Rais kwa nafasi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *