Aliyekuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye ameonesha kuguswa na tukio la kutekwa kwa mwanamuziki wa hip hop nchini Roma Mkatoliki na wenzake watatu.
Nape ambaye ni mbunge wa Mtama mkoani Lindi ametumia akaunti yake ya Twitter kwa kuandika maneno yaliyokuwa yanasomeka ‘Roma! Oooooh No!
Kwenye posti yake hiyo Mheshimiwa Nape ameweka na picha ya mwanamuziki huyo Roma ambaye kwasasa hajulikani halipo.