Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ambaye anapatiwa matibabu nchini Kenya kufuatia kujeruhiwa kwa risasi na watu wasiojulikana jana amezinduka na kutoa neno kwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.

Katika ujumbe amboa umewekwa na Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa unasema kuwa kiongozi huyo alipopata fahamu aliweza kutoa maneno machache akimtaka Mwenyekiti kuendeleza mapambano.

12_19

Tundu Lissu kwa sasa amelazwa nchini Kenya akipatiwa matibabu jijini Nairobi kufuatia kupigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa Makao Makuu ya nchi mjini Dodoma siku ya Alhamis saa saba na nusu mchana.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *