Kocha wa Inter Milan, Robert Mancini amefukuzwa kazi kama kocha mkuu wa klabu hiyo baada ya kushindwa kufanya vizuri katika msimu uliopita wa ligi kuu nchini Italia.
Inter Milan wamethibitisha kuondoka kwa kocha huyo kupitia ukurasa wao wa Twitter ambapo wamemshukuru kocha huyo kwa kuifundisha timu hiyo toka alipoanza mpaka anapoondoka.
Inter Milan imepoteza michezo yote ya kirafiki iliyocheza dhidi ya PSG, Bayern Munich na Tottonham ambapo nayo ilikuwa sababu ya kocha huyo kutimuliwa na mabingwa hao wa zamani wa Iatalia.
Timu hiyo katika msimu uliopita ilishika nafasi ya nne ambapo ilishindwa kufuzu kucheza klabu bingwa barani Ulaya msimu ujao.
Kocha wa Mabingwa wa Uholanzi Ajax, Frank de Boer anahusishwa na kuchukua nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Mancini katika klabu hiyo ya Italia.