Afisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara amewatupia lawama Bodi ya Ligi (TPLB) ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) baada ya  kubadilisha ratiba mechi ya pili ya ligi.

Manara ameeleza hayo baada ya Bodi hiyo kufanya mabadiliko ya ratiba za mechi zinazoshiriki katika Ligi Kuu ili kupisha mechi ya kirafiki baina ya Tanzania na Botswana iweze kuchezwa mnamo Septemba 2 mwishoni mwa juma hili.

Manara amesema kuwa amesikitika sana kuona kwamba ratiba ya Ligi Kuu imebadilishwa mechi hizi zipo kwenye kalenda ya FIFA.

Pia amesema kuwa wanapanga ratiba mechi ya pili tu wanaanza kubadilisha ratiba kwa hiyo mechi ya Simba na Azam FC haitakuwepo.

Manara ameendelea kwa kusema “mnatupunguza ile nguvu tuliyoanza nayo, hili jambo nilishalisema sana kwa nini mnavyopanga ratiba zenu bodi ya Ligi msiwe mnaangalia kalenda ya FIFA.

Kwa mengine mengi msikilize hapa chini Haji Manara akifunguka kuhusiana na kubadilishwa ratiba ya michuano na Bodi ya Ligi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *