Afisa Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara amendelea kulishambulia shirikisho la Soka la mpira wa miguu nchini TFF licha ya kufungiwa na shirikisho hilo.
Kupitia akaunti yake ya Instagram Manara amesema kuwa ‘Natural justice’ katika nchi hii haitambuliki kwa kuwa hakupatiwa nafasi ya kusikilizwa upande wake binafsi kabla ya kupewa hukumu.
Amendika “Natural justice nchi hii haitambuliki! wahaini na wauaji nao pia husikilizwa, iweje kwa mtuhumiwa ambaye anapigia kelele haki ya mwajiri wake?…..Ni aina ya hukumu katili zaidi kwa viwango vya mpira wetu ila nawaambia TFF Haji Manara hajawahi kuwa dhaifu wa moyo, anaweza kuwa dhaifu wa kiwiliwili lakini nina moyo wa simba nitapambana kwa kiwango cha juu sana”.
Pia ameendelea “Nitaziomba kamati zao zipokee rufaa yangu na kukaa kwa uharaka huu walionifanyia, na nipewe haki ya kusikilizwa, nisihukumiwe kishabiki wala kwa chuki”.
Vile vile Manara amesema atadai haki yake pamoja na mwajiri wake kwa viwango huku akiziomba kamati za Shirikisho za Soka Tanzania (TFF) zipokee rufaa yake.