Timu ya Manchester City imesema kuwa haina nia ya kumuuza mshambuliaji wake Sergio Aguero msimu huu wa kiangazi licha ya mshambulizi huyo kuachwa nje ya kikosi katika mechi mbili zilizopita.

Mwanasoka huyo mwenye umri wa miaka 28 alitia saini kuongeza kandarasi yake msimu huu, ikiwa na maana kuwa anasalia na miaka mitatu katika mapatano hayo.

Licha ya Aguero, kutarajia uamuzi kufanywa msimu huu wa kiangazi, viongozi wakuu wa Man City, waliashiria siku ya Jumapili kwamba, hawana nia ya kumuuza mchezaji huyo.

Mchezaji huyo wa mbele wa timu ya Argentina, alicheza dakika saba za mwisho, pale Manchester City ilipojipatia ushindi dhidi ya Swansea, baada ya Gabriel Jesus kujeruhiwa, mechi ya pili kwa mbrazil huyo, aliyechukua mahala pa Aguero katika kikosi cha kwanza cha wachezaji 11.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *