Queen Elizabeth II ni kiongozi wa taifa la Uingereza ambaye anaongoza nchi hiyo yenye uchumi mkubwa duniani.
Kiongozi huyo wa Uingereza ni tofauti sana na baadhi ya viongozi wengine duniani kutokana na kuwa juu ya sheria za nchi hiyo.
Yafuatayo ni mambo ambayo Malkia Elizabeth anaruhusiwa kufanya lakini kwa raia wa kawaida uruhusiwi kufanya nchini Uingereza na ukikaidi utajikuta jela.
1:Kuendesha gari bila leseni
Sheria hii haimtambuhi Malkia wa nchi hiyo kwani anauwezo wa kuendesha gari bila ya leseni.
2:Uwezo wa kusafiri nchi yoyote bila passport
Queen Elizabeth II anaruhusiwa kusafiri nchi yoyote duniani bila ya kuwa na passport.
3:Halipi kodi
Malkia wa Uingereza anaruhusiwa na katiba ya nchi yao kutokulipa kodi lakini aliamua mwenyewe kulipa tangu mwaka 1992.
4:Hawezi kupelekwa mahakamani
Malkia wa Uingereza haruhusiwi kushtakiwa au kupelekwa mahakani hata kwa kuua akiwa madarakani.
5:Anaruhusiwa kuendesha gari kwa speed kali.
Malkia wa Uingereza anaruhusiwa kuendesha gari kwa speed anayoitaka yeye mwenyewe bila kuingiliwa na sheria.