Mama mzazi wa muigizaji wa Bongo Movie, Irene Uwoya, Neema Mrisho amesema kuwa haitambui ndoa ya mwanaye huyo na Dogo Janja kwani ni ndoa ambayo imefungwa bila kufuata taratibu.
Mama Uwoya amesema kuwa hakufuarahishwa na ndoa hiyo kwasababu hakufuata taratibu za ndoa kama zilivyo ndoa nyingine.
Kauli hiyo ya mama huyo imekuja baada ya siku chache zilizopita Irene Uwoya kudai kuwa hakumpeleka Dogo Janja kwao kwasababu mama huyo alisafiri.
Mama Uwoya amesema kuwa utetetzi huyo hauna mashiko kwani hata kama anasafiri haiwezi kuwa mwaka mzima na kwamba, ukweli ni mtoto wake anajua wazi kuwa ndoa hiyo hawaitambui na hawamkubali Dogo kwa kuwa ni mtoto ambaye hana adabu.
Pia mama Uwoya amesema ndoa hiyo ibaki kutambuliwa na hao Irene aliowaita kuwa ni ndugu zake, waliokwenda kushiriki harusi yake na waliomfungisha na kwamba, licha ya wazazi kuwa Dar es Salaam, wanashangaa walijitokeza ndugu ambao hawawajui kusimamia jambo hilo.
Ameongezea kuwa ”Siku ambayo ndoa inafungwa ndugu zake na wazazi wake tulikuwapo lakini tulishangaa kuona kwenye mitandao kuwa amefunga ndoa na hata ilipozidi kuvuma na kumuuliza majibu yake ilikuwa kwamba, alikuwa anacheza movie hivyo tuliamua kuachana nalo kwa kuwa huwezi kumlazimisha mtu akwambie ukweli kwa kile anachokiamini yeye”.