Mama mzazi wa marehemu, Steven Kanumba, Flora Mtegoa amesema anatamani kwenda kumuona mwigizaji Lulu Michael anayetumikia kifungo cha miaka miwili jela lakini kwa bahati mbaya hawana maelewano na ndugu zake.

Flora amesema yeye kama mzazi anaumizwa na hali anayopitia Lulu na anatamani kwenda kumuona ili kumpa moyo, ila ndugu wa mwigizaji huyo wanamuona kama ndiyo chanzo cha kufungwa.

Amesema wanaomlaumu wanapaswa waelewe kwamba yeye alishasamehe kwani hata angefungwa miaka 100, haiwezi kumfanya Kanumba arudi.

“Tangu Lulu kahukumiwa nimekuwa nikipokea lawama na watu kunitusi kuwa mimi ndiyo sababu, huku wakisahau kwamba mimi nilishasamehe kama binadamu na siyo niliyekuwa mlalamikaji katika kesi hiyo isipokuwa alishatakiwa na Serikali,”

“Lakini yote namuachia Mungu kwa kuwa naamini kufungwa kwa msichana huyo hakuwezi kunirudishia mtoto wangu.”

Novemba 13, mwaka jana Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia mwigizaji mwenzake, Kanumba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *