Mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa ameipongeza mahakama kuu kwa kutenda haki katika hukumu ya Elizabeth Michael (Lulu).

Mama huyo amesema kuwa anaishikuru mahakam kumhukumu mwigizaji huyo kwenda jela miaka miwili kwa kumuua bila kukusudia mwanawe.

Pia ameongeza kwa kusema kwamba hukumu hiyo itamfanya marehemu mwanaye alale vyema zaidi kaburini mwake ambako amesema angekwenda mara moja kulitembelea leo baada ya hukumu hiyo.

Mapema leo mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam imemuhukumu kwenda jela muigizaji wa Bongo Movie Elizabeth Michael (Lulu) kwa kosa la kuua bila kukusudia dhidi ya muigizaji Steven Kanumba.

Mahakama hiyo imetoa hukumu hiyo baada ya kujiridhisha na ushahidi wa pande zote mbili toka kuanza kwa kesi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *