Mama mzazi wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Bi. Sandra amefunguka sababu ya kumpa kipigo Hamisa Mobeto.

Mama Diamond alisema hayo katika mahojiano maalum yaliyofanyika katika duka la bintiye, Esma Khan ‘Esma Platnumz’ lililopo maeneo ya Sinza Afrika Sana jijini Dar.

Mama Diamond amesema ishu hiyo ilianzia Mei 13, mwaka huu mara baada ya yeye pamoja na Diamond kutoka kwenye shoo ya msanii wa Kundi la Wasafi Classic Baby (WCB), Mbosso.

Pia amesema kwa kuwa walirudi nyumbani kwao Madale usiku, yeye alilala katika chumba chake bila kujua Diamond amelala na Mobeto chumbani kwake.

Bi. Sanda amesema kuwa kulipopambazuka, alikwenda kwenye mishemishe zake na aliporejea ndipo alipoliamsha dude baada ya kushtukia mrembo huyo amelala nyumbani hapo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *