Mama mzazi wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, mama Dangote ameendelea kuwaaminisha watu kuwa mwanawe huyo yupo mbioni kufunga ndoa.

Inasemekana kuwa Diamond Platnumz amempata mwenza ambae anatarajia kufunga nae ndoa, kama utakua mfuatiliaji mzuri wa mitandao ya kijamii Diamond alishare baadhi ya zawadi ambazo amepewa na Mke wake mtarajiwa.

Mama Dangote amepost picha na pamoja akiwa na diamond na kuandika -“Mwanangu Naseeb aliandika Mama Dangote.

Nadhani unajua kilio changu kila siku kwako, Natamani nicheze harusi yako kabla sijakata kauli Ushampata mwenza ndio umuoe Ramadhani ikiisha nawe uwe ndani ya ndoa Mwanangu….Naseeb”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *