Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake, Celestine Mwesigwa wanashikirikia na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Viongozi hao wamepelekwa Polisi kwa ajili ya uchunguzi dhidi yao kwa tuhuma za rushwa zinazowakabili.
Hayo yamesemwa na kuthibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Takukuru, Mussa Misalaba ambaye amesema taarifa zaidi wataitoa baada ya kumaliza uchunguzi wao, kwa sasa ifahamike kuwa viongozi hao wanawashikilia.
Taarifa zaidi zimeeleza kuwa Malinzi na Mwesigwa walipelekwa Sentro jana na leo asubuhi wamepelekwa Makao Makuu ya Takukuru kwa ajili ya uchunguzi kwa tuhuma zinazowakabili.
Source: Global Publishers