Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diana Exavery ‘Malaika’ amesema ametumia mamilioni kwenye urembo wa meno ili kuongeza mvuto wa tabasamu lake.

Mrembo huyo aliyetamba na ngoma kama Rarua amesema vyuma hivyo alivyoweka kwenye meno yake vimemgharimu zaidi ya shilingi milioni nne za Kitanzania na aliwekea nchini Marekani.

Kwa sasa Malaika anafanya vizuri na wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Baila mara baada ya ukimya wa muda mrefu.

Oktoba, 2017 kwenye sherehe ya 40 ya mtoto wa mwanamitindo Hamisa Mobeto, msanii Gift Stanford ‘Gigy Money’ alidai kuwa nywele alizokuwa nazo usiku huo zilimgharimu shilingi milioni sita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *