Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameweka mawikili kila wilaya kwa ajali ya kutatua matatizo ya kisheria kwa wananchi wa mkoa huo.

Wanasheria hao 35 wataanza kutoa huduma za kisheria kwa wananchi wote bure kupitia ambapo wamegawanywa katika wilaya zote za mkoa huo kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.

Mkuu wa mkoa huyo amesema hatua hiyo itasaidia kutatua kero za wananchi ambao wamekuwa na uelewa mdogo wa sheria na kusababisha wananchi hao kukosa haki zao hususani katika masuala ya ardhi,mirathi, malalamiko ya rushwa na kufukuzwa kazi na waajili wao kinyume na sheria.

Kila Wilaya itakuwa na mawakili, Kinondoni (9), Temeke (4), Ubungo (6), Kigamboni (6) na Ilala (6).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *