Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema kuwa hakuna bomoabomoa yoyote ya karne itakayofanyika ndani ya mkoa huo bila kuzingatia tarabitu za kufanya hivyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotelewa na ofisi ya mkuu huyo, imeeleza kuwa serikali imeendelea na ratiba za kurasimisha makazi.
” Mimi Paul Makonda nikiwa Mkuu wenu wa Mkoa na mtumishi wa serikali ya awamu ya tano, napenda kuwataarifu kwamba serikali hii inayoongozwa na Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli haivunji nyumba ya mtu bali inaendelea kurasimisha makazi kama ambavyo ilifanya kimara kwa kuwapatia Hati elfu Sita (6000) kwa Wananchi waliokuwa wamejenga kwenye makazi yasiyo rasmi, jitihada zinaendelea na ndivyo itakayofanyika tarehe 27/10/2017 kwa Wananchi waliojenga katika maeneo ya makongo juu,” alisema Mkuu huyo kupitia taarifa hiyo.
“Naomba niseme, na kama nimemuelewa vizuri alichokisema Mhe William Lukuvi ambae ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi ni kuwa wananchi wasiendelee kujenga bila vibali vya ujenzi jambo ambalo linawanyima haki yao ya kukopeshwa, kulipa kodi ya majengo, na mwishoni kuwa na miji isiyopangwa vizuri,”aliongeza RC.
“Naomba kukiri kuwa apo awali kulikuwa na changamoto ya upatikanaji wa vibali vya ujenzi jambo ambalo haliwezi kuwa Adhabu kwa Wananchi waliojenga miaka ya nyuma iliyopita kwani ilifika hatua Mwananchi ana Hati ya Kiwanja chake na amekamikisha michoro kwa Mujibu wa Sheria na ana fedha za kuanza Ujenzi kwa ajili ya Makazi ya kuishi, unakuta Mwananchi huyo analazimika kufuatilia manispaa kwa zaidi ya miaka miwili mpaka mitatu bila kupata kibali cha ujenzi na hata akipata kibali baada ya miaka Mitatu na kuanza ujenzi, unakuta ndani ya muda mfupi watakuja baadhi ya watu wa osha kumsimamisha kwa madai hawana taarifa ya ujenzi jambo linalotengeneza mianya ya Rushwa, akimalizana na watu wa osha Wanakuja baadhi ya watu wa kikosi cha zimamoto (fire) nao inabidi atafute utaratibu wa kumalizana nao, jambo linalokera wananchi na kuwafanya wakose hamasa ya Kutafuta vibali vya ujenzi na Hatimae kujenga kiholela,”.