Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewapiga marufuku mawakala wanaotoza faini za kuegesha magari vibaya katika kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo hadi hapo yatakapotengenezwa maeneo rasmi kwa ajili ya maegesho ya magari.
Mkuu wa mkoa Makonda alitoa kauli hiyo jana wakati alipofanya ziara kujionea hali halisi ya kituo hicho.
Alisema haiwezekani mawakala wakaendelea kutoza faini za maegesho ambayo si sahihi wakati katika eneo hilo hakuna maeneo maalumu kwa ajili ya maegesho ya magari.
Makonda pia alimtaka Mkurugenzi wa Jiji kabla ya kumalizika wiki hii kuhakikisha kituo hicho kinawekwa taa ili kuondoa usumbufu wanaokutana nao abiria na wananchi hasa wakati za usiku.
Katika hatua nyingine, Makonda amesema kuwa serikali ipo katika mpango mwisho wa kuihamishia stendi hiyo kutoka ubungo kwenda Mbezi mwisho.
Makonda amesema anataka kuihamisha stendi ya ubungo ili kuepuka kero ya kukutana na mabasi ya mwendo kasi kwakuwa nayo ni moja ya changamoto, duniani kote maroli yakiingia katikati ya mji hutumika kubeba mikate ajabu Dar es salaam maroli yanabeba ngano na makontena.