Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewapa miezi tisa wafanyabiashara wa magari jijini Dar es Salaama kuhamia Kigamboni eneo maalum lililotengwa kwa ajili ya biashara ya magari
Makonda amesema hayo leo kuwa ifikapo Oktoba mwaka huu hataki kuona mfanyabishara yoyote wa magari katika maeneo ya jiji hilo na kutaka ifikapo mwezi huo wote wawe Kigamboni.
“Ikifika mwezi huo wa tisa ambao ni mbali kweli lakini ni karibu sana, mimi akili yangu nilikuwa nafikiri niwape mpaka mwezi wa sita maanake una muda wa kujipanga saizi ila mwezi wa tisa ukiisha maanake Oktoba Mosi mwaka huu nikusikute ‘Show room’ katikakati ya Dar es Salaam”.
Aidha Mkuu huyo wa mkoa ametoa agizo kwa Afisa Biashara kuhakikisha kuwa hakuna mfanyabiashara ambaye ataweza ku ‘renew’ leseni yake akiwa mjini bali anatakiwa aweze kufanya zoezi hilo na kuhesabika yupo Kigamboni.
Pia amesema kuwa “Nimechukua majina ya wafanyabiashara wote na nakala ya leseni zao za biashara na kuanza leo na kuanzia saizi Afisa Biashara hakuna mfanyabiashara ku ‘renew’ leseni kwa ajili ya kubaki katika eneo alilopo, kama upo Magomeni uki renew unahesabika upo Kigamboni na wale wote ambao hawajachukua maeneo tafadhali jamanii hakikisheni kwamba mwezi wa tisa hatuongelei habari ya lini tuna hama”.