Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amepokea kiasi cha shilingi milioni 200 kutoka benki ya CRDB kwa ajili ya Ujenzi wa Ofisi za kisasa za Walimu jijini Dar es Salaam.

Benki hiyo imeanza kwa kukabidhi hundi ya Shillingi Million 100 leo kati ya 200 ambapo milioni mia zingine zitatolewa siku zijazo.

Baada ya kupokea hindi hiyo, Makonda amesema kuwa fedha hizo zitasaidia kununua mifuko 20,000 ya Saruji itakayosaidia kufyatua matofali 560,000 ambayo yatajenga ofisi 88 za walimu.

Makonda ameishukuru CRDB kwa kuamua kumuunga mkono kwenye kampeni hiyo ya kuhakikisha walimu wanafanya kazi katika mazingira mazuri yatakayowapa morali ya kufundisha.

Makonda amesema imekuwa ni ndoto yake kuona Walimu anathaminika ndio maana aliwapambania wasafiri bure kwenye Daladala na Treni na sasa amehamia kwenye ujenzi wa ofisi za walimu.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Bank ya hiyo, Dkt. Charles Kimei amempongeza Makonda kwa kuwa mbunifu na mwenye mawazo chanya ya kuwasaidia wananchi hususani wanyonge na kueleza kuwa wataendelea kumuunga kwenye kila jambo kwakuwa kila fedha wanayoitoa inafanya kazi iliyokusudiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *