Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amepokea Kompyuta 50 zenye thamani ya shilingi Million 85 kutoka kampuni ya ulinzi ya TAMOBA.

Akiongea wakati wa kupokea kompyuta hizo, Makonda amesema kuwa wananchi wamekuwa wakipata kero mbalimbali ikiwemo ile ya kupewa kibali na manispaa kisha wakaja watu wa zima moto wakakuzuia kuendelea kwa ujenzi sababu hawana taarifa, huku wakati mwingine ukimalizana na watu Zimamoto wanakuja watu wa OSHA nao wanakuzuia usiendelee na ujenzi.

Hivyo basi badala ya hivi vitengo husika nane kuwa sehemu moja (one stop center) badala yake vimetawanyika na kuwa kero na usumbufu kwa wananchi hasa wanaotaka kufuata taratibu.

Kutokana na sababu zote hizo Mheshimiwa Makonda ameamua kutengeneza mfumo mpya utakaomwezesha mwananchi kutokwenda kupanga foleni Manispaa yoyote ile anapotaka kibali cha ujenzi badala yake anaweza kutuma kwa njia ya mtandao na vitengo vyote vinane vikapokea taarifa hizo kwa wakati mmoja na kumfanya kila mwenye kitengo chake kuwajibika kwa wakati pasipokuwa na kisingizio cha kupoteza taarifa za wateja, urasimu na hata lugha mbaya kwa wananchi wanaotaka huduma ya Serikali.

Pia mfumo huo utamwezesha Mkuu wa Mkoa kuona nani anakwamisha utendaji ili hatua za haraka zichukuliwe na mwananchi apate huduma ya haraka.

Mfumo huu pia utamwezesha mwananchi kutuma kero inayohusu huduma ya ardhi popote alipo na ikapatiwa ufumbuzi pasipo yeye kuhangaika.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *