Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amezindua Barabara ya Bandari kupitia Kidongo Chekundu iliyopo Kurasini.

Ombi la ujenzi wa miundo mbinu ya barabara hiyo lilitolewa na Mkuu huyo wa Mkoa miezi miwili iliyopita kwa kampuni ya ujenzi ya kizalendo ya Grant Tech Company ya hapa jijini.

Barabara hiyo ina urefu wa kilomita moja na imejengwa kwa kiwango cha zege na imegharimu takribani kiasi cha Tsh. milioni 750.

Makonda amemshukuru mkandarasi huyo kwa uzalendo wake na kujitoa kwake kuijenga Dar es salaam.

Pia Makonda ametoa onyo kali kwa kampuni za ukandarasi zinazofanya shughuli zao hapa jijini chini ya viwango ya kuwa  kuanzia sasa kampuni hizo pale zitakapotambuliwa zitatakiwa kurudia miradi hiyo kwa gharama zao binafsi na kupewa adhabu ya kufungiwa kandarasi yoyote hapa jijini  kwa miaka mitatu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *