Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa siku kumi kuanzia kesho kwa Wenyeviti wa mtaa na Wazazi kuwafichua watumiaji na wafanyabishara wa dawa za kulevya.
Kauli hiyo ameitoa leo katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam wakati akizungumza na wanahabari kuhusu oparesheni ya kusaka wauzaji na watumiaji wa dawa za kulevya kwa mkoa wake.
Mkuu wa mkoa huyo amesema kuwa anatoa siku 10 kwa kila Mwenyekiti wa Mtaa kwenye mitaa yote Dar es Salaam kutoa taarifa za mtaa wake juu ya dawa za kulevya.
Pia ametoa siku 10 kuanzia kesho kwa Wazazi, kama wewe ni mzazi unaishi na mtoto anatumia dawa za kulevya na unaishi nae, njoo utoe taarif tukikukamata baada ya siku kumi na mwanao anahusika tutaamini na wewe ulikua sehemu ya kumfanya mtoto wako atumie dawa za kulevya.
Vile vile ameongeza kuwa anatoa siku 10 kwa Wafanyabiashara na Watumiaji wa dawa za kulevya, waje wenyewe Polisi kwa kamishna, kama umekua ukifanya biashara ya dawa za kulevya na umeacha njoo Polisi.