Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ameelezea ambavyo baadhi ya watu walivyotaka kupiga Tsh Bilioni 7 za serikali kwa kutaka kuwalipa watu hewa fidia za kupisha maeneo yao kwajili ya maendeleo ya miradi mbalimbali ya serikali.

Kutokana na hayo Makonda ameiagiza TAKUKURU kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua watu ambao wamehusika katika sakata hilo.

Pia Makonda amesema amepewa jukumu na Rais Magufuli la kusimamia hela ambazo zimekuwa zikitolewa na serikali kwajili ya maendeleo ya miradi mbalimbali ndani ya mkoa wa Dar es salaam.

Mkuu wa mkoa huyo amesema kuwa Katika miradi ya DMDP ambayo inahusika na barabara, ujenzi wa mifereji na uboreshaji mji wa Dar es salaam. Katika vitabu ambavyo nilitakiwa kusaini kwajili ya kupitisha hizo fedha zaidi ya tsh biloni 10 vilikuwa vitabu 31, lakini katika uchunguzi wangu na team yangu nikagundua vitabu 8 zimekiuka taratibu mbalimbali na masharti, na watu hao hawastahili kulipwa, na katika bilioni kumi tumebaini zaidi ya bilioni 5 na milioni 700 ni fedha ambazo zilikuwa zinaenda kulipwa kwa watu hewa,”.

Alisema katika wilaya Kinondoni kati ya tsh bilioni 6 na tsh milioni 600, zaidi ya tsh bilioni 1 na tsh milioni 800 zilikuwa zinaenda kulipwa kwa watu wasiostahili.

RC Makonda amedai katika jambo ambalo lilimshangaza kampuni ya mafuta ilipewa kazi ya kuthamini majengo na ardhi jambo ambalo lipo kinyume na taratibu.

Alisema katika taarifa ambapo alipewa aligundua kuna mtu alitakiwa kulipwa tsh milioni 4 kwajili ya shimo lake la taka.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *