Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amefanya ziara ya kukagua mradi wa Hospitali ya Mama na Mtoto uliopo Chanika Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam.

Makonda ameeleza kuwa mradi huo ukikamilika Mwezi Februari 2017 utaondoa hadha kwa wakazi wa maeneo ya jirani ambao walilazimika kwenda kupata huduma Hospitali ya Amana na Muhimbili.

Vile vile amefafanua kuwa Hospitali hiyo itakuwa na vitanda takribani 160 na uwezo wa kuhudumia zaidi ya wagonjwa 1000 kwa siku, huku ikiwa na vyumba viwili vya upasuaji vyenye uwezo wa kuhudumia wagonjwa wanne kwa kila chumba kimoja, na kuongeza kutakuwa na watumishi zaidi ya 150 ambao watakuwa na makazi yao hapohapo.

Katika hatua nyingine RC Makonda amewaomba wafadhili wa mradi huo ambao ni Shirika la Maendeleo la Nchini Korea (KOICA) kusaidia upatikanaji wa mradi kama huo katika Wilaya za Ubungo na Kigamboni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *