Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameikimbia kamati ya watu watano iliyoundwa na Waziri wa Habari, Nape Nnauye kuhusu sakata la kuvamia ofisi za Clouds Media akiwa na askari wenye silaha.

Hayo yamebainishwa na mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo, Deodatus Balile alipokuwa anaongea na waandishi wa habari wakati wa kukabidhi ripoti ya kamati hiyo kwa waziri Nape leo.

Balile amesema kuwa walimpigia simu mkuu wa mkoa huyo lakini hakupokea simu za kamati hiyo na pamoja na kutojibu ujumbe waliomtumia.

Kamati ikaamua kuwatafuta wasaidizi wake na wakafanikiwa kuwapata na wakaambiwa waende ofisini kwa mkuu wa mkoa huyo.

Walipofika ofisini kwake wasaidizi wa mkuu wa mkoa waliiambia kamati kuwa mkuu wa mkoa alikuwa na mgeni ambaye ni waziri wa TAMISEMI, George Simbachawene hivyo wakasubili.

Balile amesema kuwa baada ya hapo wasaidizi wake wakaiambia kamati kuwa mkuu wa mkoa anawaita na walitakiwa kupita kwenye ngazi za mbele lakini walipoenda ofisini kwake, mkuu wa mkoa akapita mlango wa nyuma na kuondoka ofisini hapo.

Kutokana na hayo kamati hiyo imejiridhisha kuwa ni kweli mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alivamia kituo cha Clouds Media saa nne na nusu usiku akiwa anaendesha gari mwenyewe lenye namba T553DFH kutokana na kitabu cha walinzi na kamera CCTV.

Kamati hiyo imejiridhisha kuwa chanzo cha tukio hilo ni kweli kituo cha Clouds kilikuwa kimeandaa habari yenye maudhui yanamuhusu Bi Grace Athumani aliyedaiwa kuzaa na mchungaji Gwajima ambapo habari hiyo ilitakiwa kuruka katika kipindi cha Shilawadu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *