Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemfariji muigizaji wa Bongo Movie, Elizaberth Michael (Lulu) baada ya kuhukumiwa kwenda jela miaka miwili.
Makonda amempa faraja hiyo kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram baada ya hukumu hiyo.
Leo mahakama ya kuu kanda ya Dar es Salaam imemuhukumu Lulu kwenda jela miaka miwili kufuatia kesi ya kuua bila kukusudia.