Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewataka viongozi wa chama cha cha Mapinduzi kurudi kwa Wananchi na kuzipatia ufumbuzi kero zinazowakabili.

Akizungumza katika ziara yake ya kichama visiwani Zanzibar, Mama Samia amesema kwa muda mrefu viongozi waliwasahau wananchi na kushindwa kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazowakabili.

 “Nimefurahishwa na utaratibu wa sasa unaofanywa na chama cha mapinduzi kuwapitia wakulima mabondeni lakini mtambue kwamba kuwa uongozi sio kukaa ofisini na kuzunguka na kiti bali ni kuwafikia wananchi ambao ndio waliowachagua”,

Mama Samia ameongeza kuwa amefurahishwa na vikundi vya wakulima wa mpunga ambavyo alivitembelea na kuahidi kuwapatia msaada mbalimbali ikiwemo trekta kwa ajili ya kuendeleza kilimo hicho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *