Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amehamia makao makuu ya nchi mkoani Dodoma.

Makamu wa Rais amehamia rasmi makao makuu ya nchi Mjini Dodoma ikiwa ni utekelezaji wa dhamira na malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano kuhamia mkoani humo.

 Samia baada ya kuwasili nyumbani kwake Kilimani Mjini Dodoma, Samia ameomba wananchi wa mkoa huo kuonyesha ushirikiano katika kufanya kazi ili kulisukuma gurudumu la maendeleo na kutimiza adhima ya serikali ya kuwaletea maendeleo wananchi wake.

Makamu wa Rais amehamia mjini Dodoma baada ya waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa kufanya hivyo mapema mwaka huu.

Baada ya makamu wa Rais kuhamia mkoani humo sasa amebakiwa Rais Magufuli kuhamia huko mkoani Dodoma ambapo anatarajiwa kuhamia mkoani humo mapema mwakani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *