Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza kuchukuliwa kwa hatua za kisheria kwa viwanda na migodi inayofanya shughuli zake za uzalishaji kwa kuharibu mazingira ikiwamo utitirishaji wa kemikali  katika makazi ya watu.

Amesema  kufanya hivyo kunahatarisha usalama wa wananchi na viumbe hai wengine. kutokana na uhalibifu huo.

Mama Suluhu Hassan ametoa agizo hilo leo kijijini Butiama mkoani Mara wakati akihutubia wananchi katika kilele cha Siku ya Mazingira Duniani.

Amesema uharibifu wa mazingira ukiachwa uendee nchini ni hatari kwa usalama wa maisha na viumbe na hivyo ni muhimu kwa viongozi katika ngazi zote kuchukua hatua zitakazosaidia kukabiliana na vitendo hivyo.

Aliongeza kuwa katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani viongozi wanapaswa kuchukua hatua za kuelimisha wananchi na kuwahamasisha ili kila mtu ashiriki katika juhudi za kuwa na uchumi unaozingatia hifadhi ya mazingira.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *