Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Januari Makamba amesema kuwa Makamo wa Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuongoza Kampeni ya kunusuru Bonde la Mto Ruaha Mkuu.

Waziri Makamba amesema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Dar es salaam.

Amesema kuwa Ofisi hiyo imeanzisha Kampeni hiyo kwa sababu Hifadhi ya Bonde la Mto Ruaha Mkuu ni kubwa kuliko yote hapa Afrika Mashariki.

Pia amesema kuwa uharibifu unafanywa kutokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu katika Bonde hilo unasababisha kukauka kwa Mto Ruaha ambao ni tegemezi katika nyanja za kiuchumi.

Makamba aliwataja Mawaziri watakaoongozana na Makamu wa Rais kuwa ni pamoja na Waziri wa Maji, Gerson Lwenge, Waziri wa Ardhi, William Lukuvi, Waziri wa Maliasili na Utalii, Jumanne Maghembe, Waziri wa Kilimo, Charles Tizeba.

Vile vile, aliongeza kuwa hali ya mazingira kwa sasa ni mbaya sana kwenye bonde hilo kwani ukifika wakati wa kiangazi mto huo wa Ruaha Mkuu hautirirshi tena maji kama ilivyokuwa zamani.

Hata hivyo alitoa wito kwa wananchi wote kutunza vyanzo vya maji, Mazingira ili viweze kuwaletea manufaa kwa sasa na vizazi vijavyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *