Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samiah Suluhu amefungua mkutano wa polisi wanawake wa Jumuia ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).
Mkutano huo unaolenga kuwajengea uwezo wa kukabiliana na matatizo mbalimbali na kubadilishana uwezo wa utendaji kazi.
Mkutano huo uliozinduliwa jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Majeshi ya Polisi Inspekta Ernest Mangu.
Mkutano huo utafanyika kwa siku tatu ambapo kuanzia kesho utakuwa ukifanyika katika kumbi zilizopo viwanja vya Mlimani City Dar.
Mkutano huo utazungumzia pia namna ya kuimarisha umoja wa SADC na kuendeleza madawati ya kijinsia katika vituo vya polisi kwenye nchi husika.