Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemwagiza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere ahakikishe anaweka utaratibu wa kukutana na wafanyabiashara mara kwa mara kama njia ya kujadili na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara hao.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere kuhusu namna bora ya kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara nchini kama hatua ya kuongeza kasi ya ukusanyaji wa kodi wa kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

Makamu wa Rais ameonyesha kusikitishwa na baadhi ya Maafisa wa TRA kuwanyanyasa wafanyabiashara na wengine kuwabambikizia kodi kubwa hali ambayo inazua malalamiko mengi kutoka kwa wafanyabiashara hao jambo ambalo amesema ni muhimu likatafutiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo.

Amesisitiza kuwa ni muhimu kama TRA itafanya mabadiliko yeyote ya ulipaji wa kodi ikawafahamisha wafanyabiashara hao mapema ili kuondoa usumbufu mkubwa unaoweza kutokea katika ulipaji wa kodi pindi wanapoagiza bidhaa mbalimbali kutoka nje ya nchi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *