Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewataka wadau nchini  kutoa ushirikiano katika kuhifadhi na kulinda bonde la mto Ruaha Mkuu.

Ameyasema hayo jana wakati wa uzinduzi wa kikosi kazi cha kuokoa ikolojia ya Bonde la mto Ruaha Mkuu iliyofanyika Mjini Iringa.

Makamo wa Rais amesema  kuwa kwa miaka ya hivi karibuni mto huo ulianza kukakuka na hivyo kuwa katika hatari kubwa ya kutoweka na kuhatarisha  hali ya uchumi wa Nchi na maisha ya mamilioni ya Watanzania wanategemea bonde la mto huo katika shughuli mbalimbali.

Aidha, amesema kuwa kutokana na matatizo mengi yanayokabili usimamizi wa hifadhi ya mazingira ya mto, baadhi ya matatizo hayo ni uharibifu wa misitu unaosababishwa na kilimo kisicho endelevu.

Ameongeza kuwa jukumu kubwa la kikosi hiko ni kuharakisha na kurahisisha utekelezaji wa sera, sheria,Mikakati na Mipango ya hifadhi ya mazingira Serikali iliyojiwekea, na kusistiza kuwa hifadhi ya mazingira na matumizi bora ya rasilimali zake ndio msingi wa maendeleo endelevu na wajibu wa kila mmoja.

Makamu wa Rais leo anatarajia kutembelea bonde la Mto Ruaha Mkuu kwa ajili ya kujionea uharibifu wa Mazingira.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *