Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameanza ziara ya siku tatu Pemba ikiwa na lengo la kuhamasisha shughuli za maendeleo.
Makamu wa Rais ambaye amewasili Pemba alasiri ya jana na kupokelewa na viongozi mbali mbali wa Serikali na Chama ambapo alipokea taarifa za mikoa miwili ya Pemba.
Aidha Makamu wa Rais aliwataka Wananchi wa Chumbageni kukumbuka historia na kurudi nyumbani,aliyasema hayo mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Tawi la CCM Chumbageni Wambaa.
Leo Makamu wa Rais anatazamiwa kuendelea na ziara yake ambapo ataweka jiwe la msingi katika kituo cha huduma za Mama na Mtoto, Shumba Vyamboni.