Naibu waziri wa afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Hamis Kigwangalla amesema kuwa atachapisha orodha ya majina ya watu anaowashutumiwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja nchini.
Kigwangalla ametetea uamuzi wake huo kwa kusema watu hawa si tu wanajihusisha na vitendo visivyokubalika katika jamii.
Lakini mwisho wa wiki katika majibishano yake na watumiaji wengine wa Twitter, Kigwangala ambaye taaluma yake ni Utabibu, alidai kwamba ushoga si swala la kibaolojia lakini ni utashi wa mtu na kwamba ni aina tu ya maisha ambayo watu wa mjini wamechagua kujihusisha kwayo.
Ameendelea kwa kutoa mfano kwamba katika vijiji vya mji anaotoka Nzega, katikati Magharibi mwa Tanzania, hakuna kabisa vitendo vya ushoga.
Hatua hii ya Kigwangalla inaambatana na uamuzi wa serikali kuvifungia vituo vipatavyo 40 vya afya ambavyo vilikuwa vikitoa huduma za UKIMWI ikiwa ni pamoja na kwa makundi ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsi moja
Mapenzi ya jinsia moja kwa Tanzania ni kinyume cha sheria na adhabu yake inaweza kuwa hata miaka 30 jela.