Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewaagiza viongozi wa Idara ya Uhamiaji kuandaa semina za mafunzo ya elimu ya uraia kwa wahudumu ya hoteli na nyumba za kulala wageni nchini ili kudhibiti wimbi la wahamiaji haramu.

Ametoa kauli hiyo mara baada ya kuwasili katika Ikulu ndogo ya Njombe na kupokea taarifa ya mkoa wa Njombe iliyotolewa na mkuu wa mkoa huo Bw. Christopher Ole Sendeka.

Waziri Mkuu amesema ni hatari kwa mkoa huo kuwa na idadi kubwa ya raia wa kigeni walioingia nchini bila ya kufuata utaratibu hivyo aliitaka Idara hiyo ijipange vizuri ili kudhibiti watu wa aina hiyo.

Katika taarifa hiyo Bw. Ole Sendeka alisema kwenye kipindi cha kuanzia Januari hadi Desemba, 2016 Idara ya Uhamiaji ilibaini kuwepo kwa raia 119 wa kigeni ndani ya mkoa huo, ambapo wahamiaji haramu 42 walikamatwa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *