Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameagiza kukamatwa kwa wazazi wenye tamaa ya fedha ambao wamekuwa wakiwakatisha masomo mabinti zao kwa ajili ya kuwaozesha.
Ametoa agizo hilo Wilayani Uyui Mkoani Tabora katika mkutano wa hadhara, ambapo amesema kuwa kuanzia sasa Watendaji wanatakiwa kuwakata na kuwafikisha katika vyombo vya dola bila woga wazazi wa binti na wale wa kijana wanakatisha masomo ya watoto wa kike kwa lengo la kuwaozesha.
Aidha, amewaonya pia vijana ambao wanamiliki na kuendesha pikipiki maarufu kama boda boda ambao wamekuwa wakiwapakia wanafunzi kwa lengo la kuwarubuni ili wajihusishe na vitendo vya ngono kuacha mara moja.
Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema mtu atakayekamatwa Serikali itamfikisha Mahakamani ili aweze kupata adhabu kali.