Watu 35 ambao ni mahujaji wamefariki dunia katika Ibada ya Hijja inayofanyika kila mwaka na kutekelezwa na Waislamu nchini Saudi Arabia katika Msikiti Mkuu mji wa Makkah.
Taarifa hizo zimetolewa rasmi na Wizara ya Afya nchini Misri, ambapo imesema kuwa siku ya kwanza ya ibada hiyo imepoteza Mahujjaji 35 kutokana na sababu ya uchovu na umri mkubwa.
Afisa mmoja wa Wizara hiyo, Ahmed el Ansary, amesema umri wa Mahujaji waliofariki ni kati ya miaka 60 hadi 85.
Katika Ibada hiyo ya Hijja mwaka huu zaidi ya Mahujaji milioni mbili wamehudhuria wakiwemo milioni 1.8 kutoka nje ya nchi.
Mahujaji hao wamekuwa wakifanya utaratibu huo wakifuata nyayo za Mtume wao Muhammad (SAW) aliyefanya utaratibu huo wa ibada kwa miaka 1,400 iliyopita.