Kiungo wa timu ya taifa ya Algeria na klabu ya Leicester city, Riyad Mahrez ameshinda tuzo ya mchezaji bora Afrika baada ya kuwashinda Sadio Mane wa Senegal na klabu ya Livepool pamoja na Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon na klabu ya Borrusia Dortmund.
Mahrez mwenye miaka 25 ameisaidia Leicester kushinda taji la ligi kuu soka England msimu uliopita.
Mchezaji huyo amewahi kushinda tuzo ya mcehzaji bora wa England sambamba na mchezaji bora wa BBC Afrika mwaka uliopita.
Mshambuliaji wa Arsenal na timu ya taifa ya Nigeria Alex Iwobi ameshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi.
Denis Onyango wa uganda na klabu ya Memelodi Sundowns akishinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa ligi za ndani.
Mchezaji bora wa kike ameshinda Asisat Oshoala wa Liverpool na timu ya taifa ya Nigeria huku timu bora ya mwaka ikiwa ni Uganda.